Bingwa Mtetezi Rafael Nadal atachuana
na Novak Djokovic katika mchezo utakaowakutanisha wachezaji wawili wa
tenesi wanaoshikilia nafasi za juu za mchezo huo duniani katika
michuano ya wazi ya Italia hii leo.
Mchezaji namba moja wa mchezo huo
Rafael Nadal aliendeleza wimbi la ushindi wake baada ya kumtoa Andy
Murray, na kumfunga Grigor Dimitrov kwa seti 6-2 6-2 kwenye mchezo wa
nusu fainali.
Djokovic, anayeshika nafasi ya pili ya
mchezo huo duniani mapema alipambana kiume na kumfuga Milos Raonic
kwa seti 6-7 (5-7) 7-6 (7-4) 6-3.
Kwa upande wa wanawake mchezaji namba
moja duniani Serena Williams atakutana na mchezaji anayeshikilia
nafasi ya 10 Sara Errani katika fainali za michuano ya Wazi ya
Italia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni