Timu ya taifa ya Argentina imemuacha
mshambuliaji wa Werder Bremen Franco Di Santo katika kikosi
kitakachocheza michuano ya Kombe la Dunia.
Kocha Alejandro Sabella
amekipunguza kikosi cha wachezaji 30 hadi kufikia 26 ambapo pia beki
wa Getafe Lisandro Lopez, beki wa kulia wa River Plate Gabriel
Mercado pamoja na beki wa Catania Fabian Rinaudo nao wamepunguzwa.
Kocha Sabella anatakiwa kuendelea
kupunguza kikosi hicho cha timu ya taifa ya Argentina hadi kufikia
wachezaji 23, ifikapo Juni 2.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni