Timu ya soka taifa ya vijana ya
Uingereza chini ya miaka 17 imetwaa ubingwa wa Ulaya baada ya
kuifunga Uholanzi kwa mikwaju ya penati 4-1 kwenye fainali
zilizofanyika huko Malta.
Kinda wa Chelsea Dominic Solanke
aliifungia Uingereza bao la kuongoza kwa shuti kali la karibu, hata
hivyo Jari Schuurman, aliisawazishia Uholanzi na kufanya mchezo huo
kuishia kuamuliwa kwa matuta.
Timu ya taifa ya Uingereza ya vijana
chini ya umri wa miaka 17, ilitwaa ubingwa huo tena mwaka 2010 dhidi
ya Hispania.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni