Lewis Hamilton amesema ni matumaini
yake timu yake ya Mercedes itapata changamoto kutoka kwa wapinzani
wao timu ya Red Bull na Ferrari katika michuano ya mbio za magari ya
Langa langa huko Monaco, mwishoni mwa wiki hii.
Timu ya Mercedes imeweza kutawala
mbio za magari katika mashindano matano ya msimu huu, na Hamilton
ameshinda mara nne, na amesema anataka kukabiliwa na ushindani mkali
ili kushinda.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni