Timu ya Taifa ya Kenya Harambee
Stars imeanza vyema kampeni za kuwania kufuzu fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika baada ya jana kuifunga Comoro bao 1-0, katika
mchezo uliochezwa kwenye dimba la Nyayo.
Katika mchezo huo wenyeji Harambee
Stars walikuwa wafunge magoli mengi lakini hata hivyo walipoteza
nafasi na kujikuta wakipata bao hilo katika dakika ya 35 kupitia kwa
Johanna Omollo ambaye anasakata soko huko Ubelgiji.
Wakati Kenya ikianza vyema timu ya
taifa ya Uganda The Cranes imejikuta ikianza vibaya baada ya kukubali
kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji Madagascar.
Uganda inayonolewa na Kocha Milutin
Sredojevic “Micho” ilipata bao pekee la ugenini kupitia kwa Hamis
Kiiza na kufufua matumaini ya The Cranes kufanya vyema katika mchezo
wa marudiano utakaofanyika Mei 31Jijini Kampala.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni