Kanye West na Kim Kardashian
wamefunga ndoa kwa kufanya harusi ya kifahari nchini Italia hapo
jana, huku Kanye akimtambulisha kwa wageni Kim kama 'my baby, Kim
Kardashian West'.
Mabilionea kadhaa waliohudhuria
harusi hiyo walishuhudia wanandoa hao wakila kiapo kwenye kilele cha
kilima katika mji wa Florence huku wakikingwa na ukuta wa kutengeneza
wenye urefu wa futi 20 uliopambwa mau, wakati jua likianza kuzama.
Wanandoa hao wapya walionekana
wakiwa wamekumbatiana kwa furaha wakiangalia wageni wao wapatao 600,
waliowaalika bila ya kuwepo rafiki wa Kanye Beyonce na Jay Z pamoja
na kaka wa Kim aitwae Rob.
Eneo la Kilimani lililofanyika harusi ya Kanye na Kim wakati likijengwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni