Mahakama Kuu ya Malawi imekataa
uamuzi wa Rais Joyce Banda kufuta uchaguzi wa mkuu uliofanyika wiki
hii, ambapo yeye pia alikuwa mgombea.
Awali Bi. Banda alisema uchaguzi
uliofanyika siku ya jumanne uligubikwa na udanganyifu, vitendo vya
upigaji kura mara mbili pamoja na kufanyiwa uharamia wa kwenye
komputa.
Rais Banda alisema kuwa uchaguzi huo
utarudiwa ndani ya siku 90 na hatogombea tena katika uchaguzi mpya.
Hata hivyo Mkuu wa Tume ya Uchaguzi
ya Malawi amesema rais Banda hana madaraka ya kuufutilia mbali
uchaguzi huo, na Mahakama Kuu imetengua uamuzi wa Rais Banda na kura
zitaendelea kuhesabiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni