Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani,
Papa Francis ametaka kumalizika kwa mgogoro usiokubalika wa Palestina
na Israel, wakati akiwa kwenye ziara yake katika Ukanda wa Magharibi
kwenye Mji wa Bethlehem.
Kauli hiyo wa Papa Francis ameitoa
wakati akikutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas ikiwa ni
sehemu ya ziara yake ya siku tatu ya Mashariki ya Kati.
Papa Francis pia aliendesha misa ya
wazi ya watu 8,000 wakristo wenyeji wa mji wa Bethlehem wa Kanisa la
Wazawa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni