.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 27 Mei 2014

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA BALOZI WA FINLAND JIONI HII IKULU


Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Finland nchini Mhe Sinikka Antilla alipokutana naye Ikulu Dar es salaam leo Mei 27, 2014. Balozi Antila ndiye Mwenyekiti wa Kundi la Nchi 12 Washirika wa Maendeleo zinazosaidia bajeti ya Tanzania (General Budget Support Group), na amechukua nafasi hiyo tangu mwezi April mwaka huu.


Lengo la Balozi Antila kuonana na Katibu Mkuu Kiongozi ni kujitambulisha kwa wadhifa huo mpya na kueleza jinsi atavyotekeleza jukumu hilo la Uenyekiti. Pia ameelezea vipaumbele walivyojiwekea katika kuchangia bajeti ya serikali na wakabadilishana mawazo ya namna ya kuimarisha mjadala (dialogue) kati ya kundi hilo la nchi washirika wa maendeleo na Tanzania.

                                                                                               PICHA NA IKULU

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni