Timu moja ya soka ya wachezaji wa
kulipwa ya nchini Bolivia imemsajili rais Evo Morales kama mchezaji
wao kiungo atakayeichezea timu hiyo katika msimu ujao.
Morales mwenye miaka 54 ni shabiki
mkubwa wa soka, na msimu ujao ataichezea klabu ya Sport Boys, yenye
maskani yake kusini-mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.
Timu hiyo ya daraja la kwanza
imesema rais Morales atakuwa anacheza soka kwa dakika 20 tu katika
mechi moja lakini si kila mchezo kutokana na ratiba yake ya majukumu
ya taifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni