Wafungwa katika gereza lenye ulinzi
mkali kaskazini mashariki mwa Brazil wamewaachia mateka 122 waliokuwa
wakiwashikilia gerezani tangu jumamosi katika mji wa Aracaju, ambao
ni mji mkuu wa jimbo la Sergipe.
Maafisa magereza wanne pamoja na
wageni waliokuwa wameenda kutembelea ndugu zao walitekwa jumamosi na
wafungwa hao na kushikiliwa baada ya kuibuka ghasi kwenye gereza
hilo.
Wafungwa hao walikuwa wanadai
kuhamishiwa kwenye magereza yenye mazingira bora na yenye kutoa muda
wa kutosha wa kutembelewa na ndugu, marafiki na jamaa zao. Katika
tukio hilo maafisa magereza wawili walijeruhiwa kidogo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni