Zaidi ya abiria 30 wamefariki dunia nchini Colombia wengi wao wakiwa watoto wenye umri chini ya miaka 14 baada ya basi walilokuwa wakisafiria kushika moto na kuteketea kabisa katika mji wa Fundacion yapata kilomita 750 kaskazini mwa Bogota.
Waumini hao wa Kanisa la Evangelical Christian Church walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kutoka katika shughuli za Kanisa hilo. Katika ajali hiyo ambayo chanzo chake bado haijajulikana, watu 18 walipatikana wakiwa hai.
Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos amesema atatembelea eneo hilo haraka.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni