Mikosi imeendelea kumuandama
aliyekuwa kocha wa Manchester United, David Moyes ambae sasa
anachunguzwa na polisi kuhusiana na ugomvi katika baa ya mvinyo
iliyopo Lancashire.
Maafisa polisi waliitwa katika baa
ya Emporium siku ya jumatano usiku baada ya mwanaume mmoja Joshua
Gillibrand kuripoti kupigwa na Moyes. Hadi sasa hakuna mtu
aliyekamatwa na polisi bado wanachunguza tukio hilo.
Kocha David Moyes alifukuzwa kazi ya
kuinoa Manchester United mwezi huu baada ya kuinoa klabu hiyo kwa
miezi 10 tu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni