Mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez
atacheza michuano ya kombe la dunia licha ya kufanyiwa upasuaji
kwenye goti, chama cha mchezo cha nchi hiyo kimesema.
Mshambuliaji huyo wa timu ya
Liverpool alipata maumivu makali wakati wa mazoezi siku ya Jumatano,
na kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha tatizo lake lililokuwa
linamsumbua.
Inakadiriwa kuwa itamchukua Suarez
kati ya siku 15 ama wiki nne kuweza kupona goti lake, wakati timu
yake ya Uruguay ikipangwa kuanza michuano ya kombe la dunia Juni 14.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni