Msemaji wa kamati ya maandalizi ya shindano la Nice and Lovely Miss Tanga 2014, Regina Gwae, akifafanua jambo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi ya mshindi wa kwanza wa shindano hilo litakalofanyika jijini Tanga Juni 21. Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Oscar Makoye na Meneja Mkuu wa Giraffe Hoteli, Evelyne Mwasela. Shindano hilo limeandaliwa na Mac D Promotions (Picha zote Francis Dande)
Ofisa Masoko wa East Africa Television Ltd, Happy Shame akizungumza wakati wa kutangaza zawadi kwa mshindi wa shindano la Nice and Lovely Miss Tanga 2014. East Africa Television ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hilo.
Meneja Mkuu wa Giraffe Hoteli, Evelyne Mwasela akizungumza wakati wa kutangaza zawadi kwa mshindi wa shindano la Nice and Lovely Miss Tanga 2014. Giraffe Hoteli ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hilo.
Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Oscar Makoye (kushoto), akizungumza wakati wa kutangaza zawadi kwa mshindi wa shindano la Nice and Lovely Miss Tanga 2014.
Msemaji wa kamati ya maandalizi ya shindano la Nice and Lovely Miss Tanga 2014, Regina Gwae (kushoto), akionesha zawadi ya gari atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza wa shindano hilo litakalofanyika jijini Tanga Juni 21. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Nice and Lovely, Brian Kelly.
Na Mika Ndaba.
Shindano kubwa la kuwania taji la ulimbwende Mkoa wa Tanga limezidi kushika kasi baada ya kampuni ya Nice and Lovely kutangaza zawadi ya gari aina yaToyota Vitz yenye thamani ya milioni10.
Shindano la kuwania kinyang’anyiro hicho litafanyika tarehe 21 Juni 2014 katika ukumbi wa Mkonge Hotel jijiniTanga,ambapo zawadi hiyo kubwa itatolewa kwa mrembo atakae ibuka na taji la MissTanga 2014 na kuwakilisha mkoa huo katika Kanda ya Kaskazini, na baadaye kuwania taji la miss Tanzania 2014.
Kufuatia muitikio mkubwa wa watanzania katika burudani hiyo ya shindano la ulimbwende, Mac D Promotions ambao ni waandaji wa Nice and Lovely Miss Tanga 2014 wamejidhatiti kuhakikisha washiriki wanakuwa na vigezo vya kuaminika ili kumpata mrembo atakae uwakilisha vyema mkoa waTanga na kuwafanya wadhamini kuendelea kushawishika zaidi katika kuyainua mashindano hayo.
Akiongea kwa niaba ya kamati ya maandalizi jijini Dar es Salaam jana Msemaji wa kampuni hiyo Regina Gwae alisema, anajivunia kuandaa shindano hilo la kusisimua na alisisitiza warembo wazidi kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi ya kipekee kwani zawadi kutoka kampuni hiyo ipo tayari na njia pekee ya kujishindia zawadi hiyo kubwa ni kushiriki ili kuonyesha kuwa unastahili.
“Pia kuna zawadi zingine nyingi za pesa taslimu kwa washindi wengine ambazo zitatangazwa baadaye. Ila cha msingi, kwa kushirikiana na Tanga Beach Resort ambapo warembo wote watakuwa kambini kuanzia June 09 hadi June 20, warembo wote wataweza kujipatia nafasi nzuri za kupata mafunzo mbalimbali yakiwemo stadi za maisha na kadhalika kutoka taasisi mbalimbali ambazo tutashirikiana nazo” alisema Gwae.
Aliongezea kuwa Fomu za kushiriki mashindano hayo zinapatikana: Mkonge Hotel, D-Boutique Tanga Mjini, Breeze Fm,Tanga Beach Resort, Five Brothers, Mwambao Fm, Sophia Records, Danny Fashion barabaraya 13, Ofisi za The Guardian Tanga barabara ya 15 ,Yolanda Salon Mtaa wa Eckenford na Nyumbani Hotel.
Mdhamini mkuu wa shindano hilo, Nice and Lovely ametoa zawadi bora kabisa ya garia Toyota Vitz ambayo inaonesha jinsi ambavyo kampuni inathamini wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Wadhamini wengine waliojitokeza katika shindano hilo mpaka sasa ni pamoja na EATV, Tanga Beach Resort, Redds, Breeze Fm,na Mwambao FM
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni