Kiongozi wa zamani wa kijeshi wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Germain Katanga atahukumiwa
hii leo baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya uhalifu wa kivita na
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Germain Katanga amekutwa na hatia na
mahakama hiyo mwezi Machi mwaka huu, na anakuwa mtu wa pili kutia
hatini na mahakam hiyo.
Katanga alihusika na mauaji ya mamia
ya wanakijiji mwaka 2003 Kaskasini Mashariki mwa DRC. Machafuko hayo
yalisambaa na kuwa ya kikabila ambapo jumla ya watu 50,000 waliuwawa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni