Mbunge wa Jimbo la Gatundu Kusini
nchini Kenya Jossy Ngugi Nyumu amefariki dunia leo akiwa nyumbani
kwake eneo la Ruanda, Jijini Nairobi.
Ngugi ambaye ni mara ya kwanza kuwa
mbunge, alianguka bafuni kwake na kukimbizwa Hospitali ya Nairobi
ambapo baadae ilibainika amefariki dunia.
Marehemu Ngugi alishinda kiti hicho
cha ubunge ambacho awali kilikuwa kikishikiliwa na Rais Uhuru
Kenyatta, kupitia tiketi ya chama cha TNA baada ya kuwashinda
wapinzani wake kwa mbali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni