Balozi Mdogo wa China Zanzibar Xie Yunliang (kushoto), akishuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Hospitali ya Abdulla Mzee Pemba kati ya Naibu Meneja wa kampuni ya JiangSu Provincial Construction Group Co. Ltd Dai Houxiang na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Saleh Jidawi. Hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar.
Naibu Meneja wa kampuni ya JiangSu Provincial Construction Group Co. Ltd Dai Houxiang akielezea mikakati ya ujenzi huo utakaoanza mwishoni mwa mwezi ujao ambao unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 25. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi. Ujenzi huo utagharimu Dola za Kimarekani milioni 13.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni