.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 23 Mei 2014

KIONGOZI WA ZAMANI WA KIJESHI DRC, GERMAIN KATANGA AHUKUMIWA JELA MIAKA 12

Kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Germain Katanga amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya uhalifu wa kivita na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).



Germain Katanga alikutwa na hatia na mahakama hiyo mwezi Machi mwaka huu, na anakuwa mtu wa pili kutia hatini na mahakama hiyo.



Katanga alihusika na mauaji ya mamia ya wanakijiji mwaka 2003 Kaskasini Mashariki mwa DRC. Machafuko hayo yalisambaa na kuwa ya kikabila ambapo jumla ya watu 50,000 waliuwawa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni