Shirika la Human Right Watch
limesema serikali ya Kenya imewarudisha kwao wahamiaji haramu 359
nchini Somalia tangu ianzishe operesheni ya kuimarisha ulinzi mwezi
Aprili 2014.
Shirika hilo limesema watatu kati ya
waliorudishwa nchini Somalia ni wakimbizi walioandikishwa.
Tarifa ya HRW iliyotolewa leo
imesema Kenya imewatimua nchini watu 98, wakiwemo watoto 12 na
kuwapeleka Mogadishu bila hata kuliarifu Shirika la Umoja wa Mataifa
la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) kuhusiana na uamuzi huo.
Mtafiti mwandamizi wa shirika la
HRW, Gerry Simpson amesema ni kinyume na sheria kuwalazimisha watu
kurejea katika nchi ambayo kunauwezekano wa kushtakiwa, kuteswa ama
kutumbukia katika hatari ya kudhuriwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni