.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 23 Mei 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA KUKAMUA MAFUTA YA UFUTA CHA TAKEMOTO, NAGOYA JAPAN


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona (wa pili kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakiongozana wakati walipokuwa wakielekea kutembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo Japan, jana Mei 22, 2014, akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini Japan. Picha na OMR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu kiwanda hicho kinavyofanya kazi hadi kupatikana mafuta ya Ufuta, wakati walipofika kiwandani hapo kujionea kutembelea na kujionea shughuli za uzalishaji, jana Mei 22, 2014. Picha na OMR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyoanza kuandaliwa kuelekea katika mashine za kukamua mafuta. Hapa ni hatua ya kwanza zinaposhushwa mbegu hizo na kuingia moja kwa moja kwenye mitambo. Picha na OMR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyosafiri hadi kufika katika Kinu cha kuzisaga hadi kupatikana mafuta hayo, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana Mei 22, 2014. Picha na OMR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mbegu za ufuta na Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana Mei 22, 2014. Picha na OMR

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni