Kiongozi aliyeng'olewa madarakani wa
Thailand Bi. Yingluck Shinawatra amefika katika jengo la jeshi mjini
Bangkok, siku moja tu baada ya jeshi kutwaa madaraka.
Bi. Yingluck ni miongoni mwa zaidi
ya wanasiasa 100, waliotakiwa kufika jengo hilo na jeshi.
Jeshi limewapiga marufuku wanasiasa
maarufu 155, kuondoka nchini Thailand bila ya kupewa ruhusa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni