Kocha Mkuu wa Harambee Stars Adel
Amrouche amesema mshambuliaji Dennis Oliech hatocheza dhidi ya Comoro
katika mchezo wa marudiano wa kuwani kufuzu michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika 2014.
Kocha Amrouche amechukizwa na
kitendo cha mchezaji huyo ambaye aliwahi kuwa kapteni wa timu ya
Harambee Stars, kutoweka katika mazoezi ya timu hiyo bila ya ruhusa
na sasa hatocheza mchezo wa Ijumaa.
Oliech, ambaye ni miongoni mwa
wachezaji wakongwe katika kikosi cha Harambee Stars, aliondoka kwenye
kambi mara baada ya Kenya kuifunga Comoro 1-0 katika mchezo
uliochezwa siku kumi zilizopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni