Mchezaji tenesi Stan Wawrinka
amekuwa wa kwanza kuonja machungu ya kutolewa kwenye michuano ya wazi
ya Ufaransa baada ya kuzidiwa kiwango na Mhispania Guillermo
Garcia-Lopez.
Wawrinka anayeshika nafasi ya tatu
kwa ubora wa mchezo huo ambaye pia ni bingwa wa michuano ya wazi ya
Australia alifanya makosa 62 na kujikuta akichapwa kwa seti 6-4 5-7
6-2 6-0.
Wawrinka, alikuwa akijaribu kuwa mtu
wa kwanza tangu Jim Courier mnamo mwaka 1992 kushinda michuano ya
Wazi ya Australia na ya Ufaransa katika mwaka mmoja.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni