Mtumishi wa ndani raia wa Ufilipino
ameachwa na majeraha ya kuungua na moto baada ya mama wa bosi wake
kumwagia maji ya moto kama adhabu ya kumcheleweshea kumuandalia
kahawa haraka.
Mtumishi huyo Fatma mwenye umri wa
miaka 23 aliachwa bila ya kupelekwa hospitali kwa saa kadhaa, licha
ya kuungua vibaya mgongoni na kwenye miguu, katika tukio hilo la
kinyama lililotokea Riyadh nchini Saudi Arabia.
Baada ya kupelekwa hospitali, alimpa
namba binamu wake mtumishi wa hospitali, ambaye alimpigia na ndipo
alipokuja kumchukua na kwa sasa yupo chini ya Ubalozi wa nchi yake
nchini Saudi Arabia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni