Mashabiki wa Pharrell Williams wa
Tehran nchini Iran wamejikuta matatani baada ya kushikiliwa na vyombo
vya dola kwa kurekodi video ya wimbo wa Happy kuonyesha furaha yao
katika taifa hilo lenye misimamo mikali ya kidini.
Video hiyo ya Happy ni miongoni mwa
video kadhaa zilizotengenezwa na wapenzi wa msanii Pharrell Williams
katika maeneo tofauti duniani katika kuonyesha furaha zao kama
maudhui ya wimbo huo yanavyoelezea.
Vyombo vya dola vya Iran vilishtukia
video hiyo iliyotumwa You Tube wakati ikiwa imeshangaliwa na watu
165,000. Tukio hili limemgusa Pharrell Williams kiasi cha ku-twitti
kwenye ukurasa wake kuwa inasikitisha kuona vijana hao wakikamatwa
kwa kosa la kusambaza furaha.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni