Wani na Mkewe Ishag siku ya harusi yao
Raia wa Marekani aliyeelekea nchi
yake ya asili ya Sudan kumuokoa mkewe mjamzito na hukumu ya kifo,
ameeleza kushtushwa kumuona mkewe huyo akiwa kwenye kizimba cha jela
akiwa na pingu pamoja na mtoto wake mdogo wa kiume.
Meriam Yahya Ibrahim Ishag,
alifunguliwa makosa ya uzinifu kwa kuolewa na mkristo Dainel Wani
raia wa Sudan mwenye uraia wa Marekani ambaye kwa sasa anaishi New
Hampshire.
Mwanamke huyo amehukumiwa pia
kupigwa fimbo 100 na mahakama ya Sudan kwa kuwa haitambui ndoa yake
ya mwaka 2011 na mumewe Wani kwa sababu Mariam Isag ni muislam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni