MMoja ya wakulima wa Mahindi Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Adalbertus Bubelwa wa pili kutoka kushoto akimwelezea Mkuu wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, jinsi alivyoandaa shamba lake. Mkuu huyo wa wilaya alikuwa katika ziara ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali wilayani humo kuangalia mazao mashambani.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, kushoto ambaye ni mwenye shamba akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Yibarik Chiza, aliyemtembelea Mkuu huyo wa wilaya shambani kwake.
Afisa Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, kulia akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima wilayani humo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni