![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg7JswFLtc8r6vG8Qe2_Lq75HgKzsUoizVmEblhPirEhyphenhyphenOFUFQDBnbo8fBp-v2ZXSxrb_xXuj2pPx8Z6HeBYz03eZgXssCW8Fx8oROphUGF7XhB8PZOPUiDqRTQArwvNZ-23w1svVe8ya5M/s1600/Wid.jpg)
Vyanzo vya habari vimesema mkimbizi huyo Muingereza amemuoa mtuhumiwa huyo mbabe wa vita Hassan Maalim Ibrahim ambaye pia hujulikana kama Sheikh Hassan, hii ikiwa ni ndoa yake ya tatu.
Sheikh Hassan ni kiongozi mwandamizi wa kundi la kikaidi la al-Shabaab ambalo linauhusiano na al-Qaeda, na sasa Samantha Lewthwaite atakuwa akipewa ulinzi mkali kutokana na kuwa ni mke wa kiongozi.
Kwa mara ya mwisho Samantha Lewthwaite alionekana katika utekaji wa duka kubwa la bidhaa Jijini Nairobi akiwaongoza watekaji nyara ambao waliua watu 67 na inaaminika waliishia kujilipua na kujitoa mhanga.
Samantha Lewthwaite ni mjane wa
mlipuaji wa tukio la 7/7 Germaine Lindsay ambaye aliuwa watu 26
kwenye treni ya aridhini huko London, Julai 2005.
al- Shabaab wakiwa mazoezini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni