Mwanamuziki nyota wa Uganda wa kundi la Goodlyfe Mowzey Radio jana asubuhi alijikuta akizolewa mzobe mzobe na polisi nyumbani kwake kufuatia ugomvi uliotokea kwenye baa ya Casablanca.
Ugomvi huo ulisababishwa na kundi la
Team No Sleep ambalo linaundwa na wasanii waliojitenga lebo ya Leone
Island ambao ni AK47 pamoja na kaka yake mkubwa Pallaso Sheebah
Kalungi na King Saha.
Kisa cha ugomvi huo ni kauli ya mmoja
wa watu wa kundi la Radio kudai kuwa kama si kwa kundi la Goodlyfe
ngoma ya AK47 na Pallaso ya Amaaso isingetamba jambo ambalo lilimkera na
kumuita kaka yake Pallaso ambaye alienda moja kwa moja kwenye meza ya
kina Radio na kuipiga ngumi.
Ndani ya gari la polisi
Mowzey Radio akiwa na Chagga, Meneja
Mpya wa Kundi la Goodlyfe
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni