Mchezaji Olivier Giroud ameonyesha
kwanini anapaswa kupangwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa
ya Ufaransa katika michuano ya Kombe la Dunia kwa kuonyesha kiwango
kizuri katika mchezo wa kirafiki na Norway Jijini Paris.
Katika mchezo huo ambao Ufaransa
iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 mshambuliaji huyo wa timu ya
Arsenal alipachika mabao mawili, huko Pogba akipachika moja na Remy
akifunga bao moja.
Mshambuliaji huyo wa Arsenal ni miongoni mwa washambuliaji watatu ambao wameitwa katika kikosi cha Ufaransa na kocha Didier Deschamps.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni