Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini
Oscar Pistorius amefika rasmi hii leo kwa mara ya kwanza katika
hospitali ya wagonjwa wa akili Jijini Pretoria ili kupimwa afya ya
akili yake.
Jaji anayesikiliza kesi yake ya mauaji
inayomkabili, alimuagiza Pistorius kupimwa hali ya akili yake kwa
siku 30 kama mgonjwa wa nje.
Uamuzi huo wa mahakama unatokana na
madai ya upande wa utetezi kusema mwanariadha huyo anasumbuliwa na
tatizo la akili yake kujawa na hofu kitaalam inajulikana kama
Generalised Anxiety Disorder (Gad).
Mwanariadha huyo amekanusha kuwa alimua
kwa makusudi mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 14, mwaka jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni