Jumapili iliyopita mshambuliaji wa timu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Cesc Fabregas alikuwa jijini London nchini Uingereza akiwa ameongozana na rafiki yake wa kike Daniella Seeman huku wakiwa katika mahaba mazito.
Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal ya Uingereza, atajiunga na wenzake wa timu ya taifa ya Hispania kabla ya fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil kuanzia June 12 mwaka huu.
Fabregas na Daniella wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye miezi 13 aitwae Lia. Hata hivyo Daniella ana watoto wengine wawili aliozaa na mtalaka wake Elie Taktout
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni