Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Brazil leo wameonja adha ya maandamano ya wananchi wanaopinga kufanyika kwa fainali za kombe la Dunia nchini humo kuanzia June 12 hadi July 13 mwaka huu.
Dakika chache baada ya kutoka katika hoteli ya Rio walikoweka kambi wakielekea mazoezini, wachezaji hao walikumbana na waandamanaji hao waliolizunguka basi lao huku wakipaza sauti kupinga fainali hizo.
Polisi walifanya kazi ya ziada kuhakikisha usalama wa wachezaji hao akiwemo Neymar, David Luiz na Hulk waliokumbana na maandamano hayo, huku waandamanaji wakilipiga kwa mikono basi walililokuwemo wachezaji hao kuelekea mazoezini.
Hii inakuja wiki tatu kabla ya kuanza kuunguruma kwa fainali hizo, huku waandamanaji hao wakipinga gharama kubwa zilizotumika kuandaa fainali hizo.
Mmoja wa waandamanaji hao akikimbia mbele ya matairi yanayowaka moto barabarani huku akiwa amebeba bendera ya Brazil katika jiji la Rio De Janeiro.
Uwanja wa Beira Rio uliopo mjini Porto Alegre ukiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Inasemekana viwanja vingi bado havijakamilika vyema tayari kwa kutumika katika fainali hizo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni