Papa Francis atatembelea eneo la
kumbukumbu ya kitaifa ya mauaji ya kikatili ya halaiki ya Wayahudi
huko Yad Vashen, katika siku yake ya mwisho ya ziara ya siku tatu
Mashariki ya Kati hii leo.
Baada ya kuwasili Israel jana, Papa
alielezea mauaji hayo ya kuchomwa moto Wayahudi yanayojulikana kwa
jina la Holocaust, kama alama isiyovumilika inayoonyesha ni kwa kiasi
gani binadamu anaweza kufanya kitendo cha kishetani.
Hii leo pia Papa Francis anatarajiwa
kutembelea maeneo ya kidini huko Jerusalem na kufanya maongezi
viongozi wakuu wa dini nchini Israel.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni