Safari za Ndege zimesitishwa kwenye
uwanja wa ndege Mashariki mwa Mji wa Ukraine, wa Donetsk baada ya
kuvamiwa na wanaharakati wanaotaka kujitenga walio na silaha.
Wanaume wengi wamewasili mapema leo
kwenye uwanja huo wakishinikiza vikosi vya jeshi la Ukraine kujiondoa
kwenye uwanja huo wa ndege.
Tukio hilo limetokea wakati ambapo
wananchi wa Ukraine wakingojea matokeo ya uchaguzi wa rais, ambapo
mfanyabiashara Petro Poroshenko anatarajiwa kushinda na kuepuka
uchaguzi wa marudio.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni