Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki
Duniani Papa Francis atashiriki katika mkutano wa kimataifa wa lishe
ulioandaliwa na Shirika la Chakula Duniani, Shirika la Afya Duniani
(WHO) na Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) utakaofanyika
Novemba Jiji la Rome nchini Italia.
Katika taarifa yake Mkuu wa Shirika
la FAO, Graziano da Silva amempongeza Papa Francis ambaye ni raia wa
Argentina kwa kutilia mkazo masuala ya mstakabali wa maisha bora ya
baadae tunaohitaji.
Mkutano huo pia utahudhuriwa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania, Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina pamoja na Rais wa
Chile, Michelle Bachelet.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni