Washambuliaji nchini China katika
mkoa wa Xinjiang wamebamiza magari mawili kwenye duka kubwa la bidhaa
na kuwaua wateja 31 vyombo vya habari vya China vimeripoti.
Pia watu hao wametupa milipuko
wakati wa shambulio hilo katika mji mkuu wa mkoa huo, wa Urumqi,
ambapo watu wengine zaidi ya 90 wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la
habari la taifa la China la Xinhua.
Wizara ya Usalama wa Raia China
imeliita tukio hilo lililotokea katika mji huo ambao ni makazi ya
kundi dogo la waumini wa Kiislam kuwa ni tukio la kikatili la
kigaidi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni