Wapelelezi wa kesi za mauaji nchini
Japan wanachunguza kesi ya msichana mmoja ambaye ameuwawa na kisha
mwili wake kufungashwa kwenye boksi na kutumwa kwa njia ya posta kama
kifurushi.
Mwili wa msichana huyo Rika Okada
umekutwa kwenye boksi la mita mbili lililoandikwa doll, yaani
kikaragosi kwenye kabati la kuhifadhia vifurushi katika Mji wa
Hachioji Magharibi mwa Tokyo baada ya kutoweka tangu mwezi Machi.
Kampuni ambayo ilisafirisha boksi
lililokuwa na mwili huo kutoka Osaka hadi Jiji la Tokyo imesema oda
ya malipo ya kusafisha boksi hilo lenye mwili ililipwa kwa kutumia
jina la marehemu Okada.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni