Jumanne, 27 Mei 2014
SERIKALI YA MALAYSIA YATOA TAARIFA SAHIHI ZA KUANGUKA BAHARINI NDEGE YAKE
Serikali ya Malaysia imetoa taarifa halisi zilizotomika kubaini ndege ya Malaysia iliyopotea ya MH370 kuwa ilianguka Kusini mwa bahari ya India.
Taarifa hizo kwanza zilitolewa kwa ndugu wa abiria wa ndege hiyo, ambao walitaka kuwepo kwa uwazi mkubwa katika suala hilo, na baadae nakala zake ndipo zikasambazwa kwa vyombo vya habari.
Nakala za taarifa hiyo zilizotolewa leo zina ukurasa 47 za taarifa, pamoja na maandiko ya kampuni ya Uingereza ya Inmarsat.
Ndege ya MH370 ilipotea Machi 8 ikitokea Kuala Lumpur kwenda Beijing ikiwa na abiria 239 wengi wao wakiwa raia ya China.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni