Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria
amelaani tukio la milipuko miwili ya mabomu katika mji wa Jos ambayo
imepelekea kutokea vifo vya watu 118.
Rais Jonathan amesema wale
waliotekeleza shambulio hilo ni wakatili na wanaroho za kishetani.
Inahofiwa kuwa miili zaidi bado
imefukiwa kwenye kifusi cha majengo yaliyobomolewa na milipuko hiyo
ambayo ililenga soko lenye watu wengi na hospitali.
Rais huyo amesema amejidhatiti
kupambana na magaidi licha ya kukosolewa kuwa ameshindwa kuimarisha
usalama katika nchi ya Nigeria.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni