Meneja mpya wa Manchester United
Louis van Gaal anataka kuendeleza historia yake nzuri akiwa na timu
ya Barcelona na Bayern Munich, kwa kushinda Ligi Kuu ya Uingereza
katika msimu wake wa kwanza.
Kocha huyo alishinda kombe la La
Liga mwaka 1997-1998 akiwa na Barcelona kabla ya kutwaa kombe la
Bundesliga akiwa na Bayern Munich.
Hadi sasa ni makocha watatu tu
waliowahi kushinda Ligi Kuu ya Uingereza katika msimu wao wa kwanza
ambao ni Jose Mourinho akiwa na Chelsea, Carlo Ancelotti na Manuel
Pellegrin wakiwa na Manchester City.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni