Mshambuliaji wa Real Madrid mwenye kasi kali uwanjani, Gareth Bale akiwa amelinyanyua juu Kombe la ligi ya mabingwa Barani Ulaya baada ya kulitwaa jana usiku katika mchezo uliochezwa dakika 120 ili kumpata mshindi.
Ligi ya mabingwa barani Ulaya ilifikia kilele jana usiku mjini Lisbon, Ureno kwa kushuhudia fainali kali iliyozikutanisha timu toka mji mmoja na nchi moja.
Real Madrid na Atletico Madrid zote toka Hispania, zilipambana kiume jana ili kuamua bingwa wa kombe hilo lenye thamani kubwa kabisa barani Ulaya.
Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Atletico Madrid wakitangulia kufunga kunako dakika ya 36 kupitia kwa Godin, hata hivyo Real Madrid walisawazisha bao hilo kunako dakika ya 90 kupitia kwa Ramos.
Kufuatia kumaliza dakika 90 timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, ilibidi ziongezwe dakika nyingine 30.
Ni katika muda huo wa ziada Real Madrid walipowapa kichapo kikali Atletico Madrid kwa kuwazamisha kwa mabao mengine matatu ya haraka haraka wafungaji wakiwa ni Balle dakika ya 110 kwa kichwa safi kabisa, Marcelo naye akifunga bao la tatu dakika ya 118 kabla ya mchezaji bora wa mwaka, Cristiano Ronaldo kufunga bao la nne nala ushindi kwa mkwaju wa penati dakika ya 120.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni