Ripoti ya dunia ya unywaji wa pombe
duniani iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonyesha kuwa
Kenya inaidadi ndogo ya walevi, kuliko nchi jirani za Tanzania,
Rwanda, Malawi na Burundi inapokuja suala la soko la pombe katika
ukanda huo.
Ripoti hiyo ya WHO inaonyesha kuwa
soko la pombe Kenya linafikia asilimia 20, ikilinganishwa na asilimia
89 nchini Uganda, asilimia 87 Tanzania na asilimia 17 nchini Afrika
Kusini.
Takwimu za ripoti hiyo Hali ya
Unywaji Pombe na Afya ya mwaka 2014, zinaonyesha asilimia 23.1 ya
wakenya hunywa pombe, miongoni mwao asilimia 5.2 hunywa kupindukia,
ikilinganishwa na Rwanda asilimia 44.7 hunywa pombe, Tanzania
asilimia 41.8, Burundi asilimia 41.1 na Uganda wanywaji wa pombe ni
asilimia 41.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni