Seneta Sonko akiwa katika pozi na mbunge Rachael Shebesh
Seneta wa Jiji la Nairobi Mike Mbuvi
Sonko amedai kuwa maisha yake yapo hatarini kufuati madai ya kuwepo
kwa ugomvi baina yake na Mbunge Mwakilishi wa Wanawake Rachael
Shebesh katika baa moja siku ya jumamosi.
Seneta huyo ametoa madai hayo kwenye
ukurasa wake wa Facebook, saa kaadhaa kupita tangu kutokea kwa ugomvi
huo ambao uliambatana na kufyatuliwa kwa risasi. Sonko aliandika
taarifa yake katika kituo polisi cha Kilimani usiku huo huo wa tukio.
Wanasiasa hao wawili wameagizwa
kuripoti Ofisi ya Mpelelezi wa Makosa ya Jinai katika kituo cha
Kilimani hii leo.
Wakati hayo yakijiri picha
zinazomuonyesha Seneta Soko na Mbunge Shebesh wakiwa wamekaa katika
pozi linaloashiria kuwa na uhusiano wa karibu mno zimekuwa
zikisambwazwa kwenye vyombo vya habari.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni