Mchezaji tenesi Victoria Azarenka
amethibitisha kuwa ataikosa michuano ya wazi ya Ufaransa.
Mchezaji huyo anayeshika nafasi ya
tano ya mchezo huo duniani, bado anapona jeraha la mguu wake
lililomlazimisha kujitoa katika michuano ya Doha, Miami, Madrid na
Rome katika wiki za hivi karibuni.
Mchezaji huyo raia wa Belarus,
ametoa taarifa ya kutoshiriki michuano ya wazi ya Ufaransa kupitia
ukurasa wake wa Twitter.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni