Timu ya Barcelona imemteua Luis
Enrique kuwa kocha wao mpya atakayekinoa kikosi cha kwanza cha timu
hiyo kwa miaka miwili.
Kocha huyo aliyewahi kuichezea
Barcelona, ambaye pia aliwahi kukinoa kikosi B cha timu hiyo kati ya
mwaka 2008 na 2011, anatokea klabu ya Celta Vigo.
Kocha huyo anachukua nafasi ya
Gerardo Martino, ambaye anaondoka Barcelona baada ya kushindwa kutwaa
kombe la ligi ya Hispania na kuishia kushika nafasi ya pili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni