.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

ABIRIA AHOFIWA KUWA NA MAAMBUKIZI YA EBOLA, NI BAADA YA KUTAPIKA DAMU NDEGE IKIWA ANGANI

Ndege iliyokuwa ikisafiri kutoka Sydney kuelekea Darwin ikiwa na abiria 140 ndani jana jumatano ilibidi kugeuka na kurejea tena mjini Sydney saa moja tu baada ya kuwa imeruka angani baada ya abiria wake mmoja mwanaume kuanza kutapika damu ndege ikiwa angani, hali iliyozua taharuki kwa abiria wakihofia kuwa abiria huyo uhenda ana maambukizi ya virusi vya Ebola.
Msemaji wa shirika hilo la ndege alithibitisha abiria huyo kupatwa na hali hiyo na kukanusha kuwa uhenda hizo ni dalili za abiria huyo kuwa na maambukizi ya uginjwa wa Ebola. 

Abiria huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu, na abiria wote walishushwa katika ndege na wengine kusubiria hotelini kw amuda kabla ya kuendelea na safari yao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni