Mshitakiwa anayedaiwa kushiriki katika mauaji ya mke wa mfanyabiashara wa Uingereza, Shrien Dewani amedai mahakamani kuwa alipata ujumbe kuwa kuna mfanyabiashara ambaye anatafuta mtu atakayefanikisha mauaji ya mkewe.
Mtuhumiwa huyo Mziwamadoda Qwabe raia wa Afrika Kusini, alitoa madai hayo katika mahakama kuu nchini Afrika Kusini wakati akaitoa ushahidi wake.
Mtuhumiwa huyo tayari anatumikia kifungo cha miaka 25 gerezani kwa kukiri kumuua Anni.
Dewani mwenyewe amekuwa akikanusha kumuua mkewe na kusisitiza kuwa tukio hilo la kuuliwa mkewe ni baada ya kutokea utekaji nyara katika jiji la Cape Town.
Mtuhumiwa Mziwamadoda Qwabe anayedaiwa kumuua Anni Dewani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni