Rais Uhuru Kenyatta jana alihudhuria mahakamani kusikiliza mashitaka yanayomkabili ya uchochezi wa machafuko ya kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 yaliyosababisha vifo vya zaidi ya Wakenya 1,200 huku wengine wakikimbia makazi yao.
Katika kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi duniani, Rais Kenyatta anakuwa kiongozi wa kwanza kuwa madarakani kufika mbela ya mahakama hiyo.
Kupitia wakili wake Stephen Key, Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akikanusha madai hayo na kuitaka kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni